Tuesday, September 28, 2010

PFUNK NA AFANDE WAYAMALIZA MATATA YAO...

Wawili hawa walizungumza na kipindi cha HITS VIBE ZONE ..na wakasema kua hakukua na beef kama vyombo vingi vya habari vilikua vimesema hapo awali,espokua kulikua na kuto elewana katika pande zote mbili lakini ...lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa coz wawili hawa wapo kama ndugu.pfunk anajianda na ziara yake ya nchi mbali mbali barani ulaya na amerika kati ka mda mfupi ujao..na pia pfunk kasema kua sasaivi mambo yamebadilika kidogo kutokana na mda wa kuka na kufikiria kabla ya kuachia kazi.na vile vile umri wake pia umemfanya awe na mtazamo tofauti na zamani...kwa upande wa Afande.amesema kuwa anamtambulisha  msani wake bwana Ballet wallet..ambaye amefanya naye kazi ya SUZI..


Wednesday, August 18, 2010

WYCLEF JEAN AMEJIFICHA BAADA KUPOKEA UJUMBE WA KUTISHIA MAISHA YAKE.

Mwana muziki wyclef jean tokea nchini Haiti ameingia chimbo isiojulikana pamoja na familia yake maara baada kupoke ujumbe unao mtishia maisha. inasemekana kua kuna watu walimtumia Wyclef ujumbe unao mwambia ahame faster kisiwa hicha cha Haiti kabla hawaja mfanyia kitu kibaya. kuna watu walisema kuwa haiwezekani mwana muziki huyo kuwania urais kwa kuwa haja kaa nchini humo kwa mda wa takribani miaka 5 mfululizo,lakini kwa upande wa msemaji wa Wyclef,amesema kuwa jama  ni mmiliki wa kituo cha television nchini Haiti na alikua analipa kodi zake za vizuri na alikuwa akirudi mara kwa mara nyumbnani.so hadi hapo ana haki zote za kuwania ubunge..
Hiyo ime onyesha waazi kuwa kuna watu ambao hawaja furahia nia ya mwana muziki huyo kugombea urais nchini humo. hadi sasa kuna wagombea zaidi ya 30 ambao wametangaza nia ya kuwania urais..miongoni mwa hawa yupo mjomba yake Wyclef.
lakini kwa sasa hadi atakavyo toka chimbo, hakijaeleweka kama ataendela na nia yake ya kuwania ubunge maara baada kupokea vitishio hivyo..

Monday, August 16, 2010

PROMOTER SADAT AMTOSA RAYC NA KWA SASA ANATAKA KUMPA DEALI K-LYNN

Promoter(Sadat Muhindi) alie mpa Ray c deal ya ku promote kinywaji kipya kiitwacho DASH ENERGY DRINK ndani ya nchi kenya.shavu la promo amelitupa kwa mwana dada mwengine K-LYNN..haya yote ni baada kuto elewana yeye na Ray-C .upande wa Ray-c anasema jama alimtaka ki mapenzi ,ndio maana hakukua na maelewano.lakini pia jama promoter Sadat,naye ana story yake tofauti..so inasemekana yeye (Sadat)na K-LYNN wapo kwenye mazungumzo ...deali la kupromote kinywaji hiki, lina mpunga wa kiasi cha million za kenya mbili nukta tano(2.5 million kshs)

THE KOKOMASTER aka DBANJ KUTUA NDANI YA JIJINI NAIROBI KWAJIRI YA CONCERT MAARUFU KAMA NAIJA NIGHT MWEZI WA KUMI..

mkali wa FALL IN LOVE toka nchini Nigerian anajulikana zaidi kama Dbanj..atakwepo kati ka usiku wa NAIJA NIGHT nchini humo mmwezi waku kumi (oktoba)..hayo amesema mwanzilishi wa usiku huo   Iyke Anok..ameogezea kwa kusema kuwa yeye na kampuni yakwapo kati ka jitiada nyengine ya kumpata mwigizaji maarufu GENEVIVE NAJI alie kuwa kwenye shooting ya wimbo  wa DBANJ "fall in love" aunganike na KOKO MASTER aka Dbanj ndani ya show ya usiku huo maarufu kama NAIJA night..

KIBA AUWA UVUMI WA KUWA ANA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA MWANAE RAIS WA SUDAN


uvumi huo ulianza kwenye mitandao mbali mbali kati ka nchi tofauti za africa masheriki..inasemekana kuwa mwanzo ulikua kule nchini kenya KIBA alivyo enda kuburidisha raia wa nchi hiyo..mwana dada huyoalivyo skia KIBA yupo pande hizo aka amua kumtimbia huko huko Nairobi...lakini KIBA ameweka wazi kua yule mwana dada sie mtu wake espokuwa ni marafiki na kipenzi chake.KIBA alikiri kweli alikuja Nairobi lakini kwa lengo la kuonane na rafiki yake ambae ni kipenzi changu..hAya yote KIBA aliasema akizungumza na chombo kimoja cha habari jijini Nairobi juzi kati.

Tuesday, August 10, 2010

LIL KIM NA NATURE KWENYE TRACK

BUSU LA SHAVU KUTOKA KWA KIM KWENDA KWA NATURE LIME ZAA MATUNDA..KWA SASA KUNA UVUMI KUWA NATURE ATALIPUA KITU CHA PUNCH NA MWANA DADA TOKA BROOKLYN NEW YORK.

Wednesday, August 4, 2010

HAPPY BIRTHDAY PRESIDENT OBAMA NA VILE VILE MAMA WA MSISIMKO ...SAMIRA SULEIMAN

Shavu la kutosha kwake samira suleiman kwa kuweza ku share birthday na mtu mzima rais wa Marekani  Barrack Obama..mtu mzima Obama anatimiza 49 wakati mwenzetu Samira anatimiza..mmm...mmmh....dah ! amekata kutoa umri wake bana...lakini yote sawa happy birthday kwenu nyote ambao pia mme zaliwa siku mhimu kama hawa wawili..

Monday, August 2, 2010

Tamasha la KWANZA LA watoto lafanyika bagamoyo agosti mos 2010


Tamasha la watoto la kwanza limeandaliwa na jama au mwite msani wa muziki wa asili bwana Vitalis Maembe..Maembe amefanyikisha tamasha hili bila msada wowote.kutoka nje au kwa serikali.espokua waalimu wanaofundisha vikundi mbali mbali vya sanaa kati ka vituo tofauti tofauti..

Tamasha hili la watoto limefanyika kwa mara ya kwanza siku ya jumapili ya tarehe mos mwezi wa nane mwaka huu wa 2010 ndani ya bagamoyo.

maonyesho yalifanyika katika ukumbi wa mwembeni ndani ya chuo cha sanaa.walio shiriki ni watoto kutoka vituo mbali mbali vinavyo toa elimu ya ziada kwa kusaidia kuongeza maarifa katika maisha ya watoto hawa .hayo yote yalifanyika ndani ya bagamoyo.

watoto hao walionyesha sanaa zao za kuimba na kucheza muziki wa utamaduni wa tanzania...

picha kutoka katika ka tamasha hilo                             muanzilishi wa tamasha la watoto (MAEMBE)





Thursday, July 29, 2010

CHAMELEONE AMPA KICHAPO MDOGO WAKE MAURICE KIRYA" VAMPINO "......

Watu wengi wamezungumza..juu ya kitendo cha mwanamuziki jose chameleone kumpiga msani mwenzake tokea nchini uganda aitwae VAMPINO .hayo yote yalifanyika siku ya j5 nje ya club silk ...kiwanja maarufu nchini humo cha muziki.inasemekana kuwa chanzo ni kwaNINI Vampino hamkubali jama..kwa hiyo ye chameleone anaona  kama jama anamdharau.wengi wanasema kuwa huyu jama (chameleone) tabia yake sio nzuri..tangu apate fursa ya kuonyesha sanaa yake kwenye jukwa wa la kombe la dunia..
Vampino alilazwa hospitali kansanga na watu wake wamefungua kesi dhidhi ya jose chameleone katika kituo cha police  jinja road...

badhi ya watu tokea nchini humo wamesema haya kupitia mtandao wa urafiki facebook..

kaka yake Vampino bwana Maurice kirya ambae pia ni msani kasema haya

"

I was blind but now i see, with blows to his face, he wondered why he
was attacked,and the answer was,because he did not worship the Dr.
Joseph chameleon! i hope my brother vamposs recovers from the injuries
and dis figured face, i love his music, but chameleon has attacked many,
and is protected by all of us. We have ..."


mtu mwengine ambae ni mtangazaji wa kituo cha redio hot 100 jijini kamapala kaesema haya
bwana 
"

Banange Chameleon...wateva they say u did to My boy Vampos was such a cheap shot. I love yo music bt smthangz take the love away."

Tuesday, July 27, 2010

MAPENZI NDANI YA BIG BROTHER TAYARI

Kulikuwa na habari kuwa Sheila kutoka nchini Kenya na Hanningtone kutoka uganda walikuwa na kiji issue flani cha mapenzi kilicho kuwa kinaendelea..Kwa kuweka mambo sawa Sheila alikata kabisa swagga hizi za kuwa ana feel lolote kwa chali huyo kutoka uganda na hapo baadae aliskika jama Hanningtone akiwa anamlalamikia kwanini alimvunja moyo...duh ! hii kali..na kwa habari nyingine ,siku ya jana (j3)Tatiana alitolewa (kwa maana ya kwamba she was voted out like eviction) kwenye jumba la B.B.A...lakini..akarudishwa tena..

NYOTA WA MUZIKI MWENYE ASILI NA CHIMBUKO YA NCHINI HAITI AMETANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAISI

wycleff jean anae ishi nchini marekani kwa sasa ,ametangaza nia ya kugombea cheo cha uraisi..nchini haiti..kwa saivi ni balozi wa Haiti nchini marekani lakini nia yake anasema ilianza mwaka 2007 wakati alivyo teuliwa kuwa balozi wa nchi Haiti...Japokuwa raisi aliopo madarakani kwa sasa Rene Preval hana nia ya kugombea tena,Wycleff kasema ye binafsi ataendelea kutoa misada kwa watu wake wa Haiti na kuwa karibu nao katika kipindi hichi kigumu walicho nacho kwa sasa....




LAURYN HILL NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

Msani wa kitambo alie tikisa sana ulimwengu wa mziki miaka ya tisini..Lauryn Hill alikua nchini Rwanda siku ya juma pili ambapo alitupi bongela show Katika tamasha la FESPAD..kama ilivyo kawaida walikwepo wakali wengine kama jose chameleone toka nchini uganda na pili pili toka nchini Kenya NA WENGINEO KIBAO..

Kilicho shangaza zaidi ni kwamba ame achia ngoma yake mpya(REPERCUSSIONS) nchini humo (KIGALI)hata kabla ya kuiachia marekani anapotokea mwana dada huyo..na pia miss Hill ata tupi performance kwenye tamasha lingine nchini marekani linalojulikana kama ROCK BELLS

Sunday, July 25, 2010

HII KALI..TUNAFAHAMISHWA KUWA JIGGA ANASAFIRI NA TOILET PAPER YAKE SPECIAL KILA SEHEMU AENDA KO

Mwana muziki toka kasabia Tom Meighan, ameeleza  kwanini hajahisi kama ye ni maarufu,miongoni ni kuwa ,hajapata toilet paper zake na choo kama jayz.jama vile vile anasema akibahatika kuwa na hivyo vitu hapo basi naye atajijua kama ni nyota na ni maarufu..


 .inasemekana kuwa Hov kila anapo safiri ku perform kwenye festival mbali mbali uwa ana burungutu la toilet paper na private toilet. HOV anasema kwenye mistari ya kinyamwezi kuwa ana shida 99..ila kumwabukiza wadudu wako sio moja ya shida hizo...


"

"I Got 99 Problems & Your Germs Aint One: Jay-Z Takes Private Toilet With Him Everywhere"

fiesta ipo home kwetu zanzibar....

MWENZETTU LUIS KOLUMBIA AKIUZURIA MKUTANO WA WAGOMBEA

Friday, July 23, 2010


VODACOM FOUNDATION KUDHAMINI GALA NIGHT ZANZIBAR


Meneja wa Mfuko wa Vodacom fondition, Yessaya Mwakifulefule 8kushoto na mbunifu wa mavazi Mstapha Hassanali wakizungumza na waandishi wa habari

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na mbunifu wa mavazi Mstapha Hassanali imejitokeza kudhamini maonesho ya mavazi ya hisani yanayolenga kuboresha hali ya mazingira ya Hospital ya wenye matatizo ya akili ZANZIBAR.

Maonesho hayo yanayofahamika kama 'Fashion 4 Health Black and Gold Gala' yanafanyika mara ya tatu mfururizo yanaandaliwa na Exprlore ZANZIBAR yatafanyika tarehe 30 Julai mwaka huu katika Hotel ya Serena Inn Mjini humo.

"Kwa kuthamini umhimu wa jamii ambayo tunafanya nayo kazi na kwa Heshma ya Maryam Olsen wa Explore Zanzibar tumeshawishika kudhamini onesho hili kuchangia majengo ya Hospitali hiyo," alisema Mwakifulefule.

Naye mbunifu maarufu wa mavazi nchini Mstafa Hassanali alisema katika maonesho hayo atazindua mtindo wake mpya wa mavazi unaofahamika kama 'KARAFUU Collections', akiambatana na wanamitindo wengine 10 kutoka Tanzania bara wakisindikizwa na burudani kutoka katika bendi ya Tanzanite.

Alisema mbunifu mwingine wa Mavazi Farouque Abdella wa zanzibar atafungua pazia la maonesho hayo akifuatiwa na mbunifu Mago ambapo wadhamini mbalimbali wakiwemo PSI Tanzania, 361 degree Events na Mstapha Hassanali Couture wamejitokeza kudhamini maonesho hayo.

"Wagonjwa wana kila sababu ya kujifunza na kuishi katika mazingira ya kupendeza lakini tunahitaji msaada na mimi kwa kushirikiana na wenzangu tutashiriki kikamilifu katika onesho hilo kuchangisha fedha," alisema hassanali.

UZINDUZI WA MSANI AT KUKUSANYA WASANI NYOTA TOKA TANZANIA NA KENYA

miongoni mwa wasani watakao kwepo ni, Shiko,Mheshimiwa temba, ali kiba, berry black, hussein machozi, baby j, doricah, jelly wa rhymes, black, k.r. kutoka   tmk, nyota ndogo kutoka mombasa...

Tuesday, July 20, 2010

MWISHO MWANA KUTOKA MO TOWN KAREJEA BIG BROTHER AFRICA

Chali ka'amua kurudi big brother kuonyesha ma skillz yake..alikwepo na afro mwanzoni lakini mara hii, amengia na kipara..so tayari amesha onyesha mabadiliko kati ka maisha yake..hehehehehe.. tumsubirie kwa sana tuone swagga za mara hii..

Friday, July 16, 2010

KUMBE KRE-GALS HALISI HAWA KWEPO KWENYE VIDEO YA TEACHER.

siku ya jana (alkhamis ) kabla ya bongela show walio tupia pale NGOME KONGWE KRE-GALS wali weza kudondoka kwenye mjengo wa Hits fm radio hapa zanzibar.

wakiwa na prodyuza wao LAMAR na msani mwenzao YOUNG DEE. kitu ambacho walizungumzia ni kuwa hawakupata nafasi ya kushiriki kwenye video ya wimbo wa Young Dee  "TEACHER" kwa sababu walikua busy na skonga..so watu wengi wakafikiria kuwa wale kwenye video ya teacher ndio kre-gals,kumbe sio. so siku ya jana wali weka wazi hilo na kulitolea ufafanuzi kiundani zaidi.

kikali zaidi ni kwamba kuna pini jipya ambalo waliweza kulitambulisha ndani ya kipindi cha "POWER ENTERTAINMENT RELOADED"

KRE-GALS wanatambulika  kwa majina yao mengine ambao  mmoja wao ni "TATA" na mwengine ni "YOYO"  na jina la ngoma yao mpya ni "SITARUDIA"ambao wameshirikiana na mkali wa  michano Binamu a.k.a Mwana F.A..lakini pia Young Dee, alituachia mzigo wake mpya...hayo yote ndio mambo ya FISH CRAB !!!

MR.BLUE AULIZA SWALI ,DIVA NDIO NANI..?

Siku za nyuma kidogo kwa wewe ambae ulikua haufahamu ni kwamba kuna mwana dada anaitwa Diva .habari zilianza kuvuma kuwa Blue anamsumbua .sasa kwa upande wake .Blue anasema mimi simjuhi huyo DIVA (mtangazaji wa kituo kimoja cha redio jijini dar-es-salaam)lakini kitu kinacho nishangaza ni kwamba, naskia habari zina vuma kati ka vyombo vya habari mbali mbali hapa nchini kuwa mimi BLUE ninamsumbua huyo DIVA .kitu cha kwanza hatujawahi kukutana mi na yeye. sasa watu wanavyoandika hizo habari sijuhi wanazitoa wapi.
Ni hayo tu ! kutoka kwa Blue a.k.a KABISA...ila kwa misemo ya siku hizi ni kwamba itafahamika tu !!
.

Thursday, July 15, 2010

MKALI WA CAKE ISIO OZA (ALBINO FLANI )NA MSANI WA KIKE PIPI WAMETUPIKIA KITU KIKALI

Mchizi huyu anae kwenda kwa jina la kimziki kama Albino fulani yupo unyamwezini (marekani) ambapo yupo based ki maisha na kazi.hili goma jipya waliotupikia na mwana dada PIPI mara hii linakwenda kwa jina USIHOFU .. la  Fulani yuko mbioni kutoa album ambayo mapato yake ataelekezea katika kusaidia Maalbino wenzake kama mchango na chachu ya kuamsha albino wenzake kuwa wasikate tamaa na maisha kwani nafasi bado wanayo kama alivyowaambia kwenye track yake iliyopita ambayo alimshirikisha MwanaFa, Belle9, & Sugu.


Hivi karibuni Albino Fulani alitoa misaada ya lotions za kinga za jua kwa maalbino wenzake Tanzania kupitia shirika lisilo la kiserikari la Afrobino.org katika jitihada zake za kupambana na Cancer ya ngozi.

hapokweli ndio unaona bidi ya mchiz.jama  yupo serious na anthamini kweli ndugu zake hawa.pamoja sana kaka umoja ni nguvu

marafiki zetu walio tutembelea ndani ya wiki mbili hizi...

Tuesday, July 13, 2010

HATIMAE PINGU ZA MAISHA ZAFUNGWA KATI KA MARTIN LAWRENCE NA MPENZI WKE WA MDA MREFU..

Jama alie jijengea umaruufu kwa kuigiza kama komedian hatimae ameamua amuoe mpenze wake wa mda mrefu..tukio hili limefanyika kisiri kama ilivyo siku zote kwa watu maarufu nchini marekani..ka sherehe haka kalikuwa ka waatu maaluum tu.

jama alifahamika sana kwa movie Zake alio i cheza na chizi mwenzake will smith. (BIG MOMMA'S HOUSE 1&2, BAD BOY 1 & 2) Lakini pia ana movie nyingine pia ambao ni nzuri sana, zikiwemo..THIN LINE BETWEEN LOVE AND HATE alio i cheza na mkongwe mwengine katika anga za filamu Angella Bessette,RASCOE JENKINS na nyingine kibao...

Saturday, July 10, 2010

CHAMELEONE NDANI YA SAUZ NA MKE WE .ATATUMBWIZA J-PILI SAA MOJA KAMILI JIONI

msani huyo toka nchini uganda amesha tua sauz akiwa na mke we Daniella .amekutana  na wasani mbali mbali toka hapa barani afrika,kama 2face,samini na wengine toka bara la marekani kama shakira .wasani hawa ni miongoni mwa wale ambao wanatakiwa kutupia bongela show la kufunga kombe la dunia nchini humo.

KULIA NI CHALI AKIWA NA WIFE WAKE DANIELLA..


HAPA MWANA NA WAKALI WENGINE
TOKA NCHI MBALI MBALI NDANI NA NJE YA AFRIKA AMBAO PIA WAPO KWA AJILI YA KUTUMBWIZA NDANI YA SOCCER CITY.
MAMBO YA KUOMBANA KUPIGA PICHA NAYO YALI KWEMO ..HAPO MKE MTU AKIPIGA PICHA NA SHAKIRA NA VILE VILE MME MTU NAYE AKIZUGA
LAKINI MPANGO WAKE PIA TULI UJUA . NAOMBA
 TUPIGE PICHA YA KUMBUKUMBU..

KUMBE MASTAR NAO WANA SWAGGA HIZO ZA KUTAKA WAPIGE PICHA NA MTU ALIE JUU YAKE
HEHEHEHEHEHEHEHE...!!!

Thursday, July 8, 2010

RECOVERY TAYARI IMETINGA PLATINUM

jama toka PANDE ZA Detroit nchini marekani almarufu kama EMINEM a.k.a Marshall mathers,tayari ameshafikisha mauzo ya PLATINUM manake mauzo ya cd zaidi ya millioni moja na laki moja (1,100,000)ya album yake mpya RECOVERY.album hii ilingia sokoni mda wa kama wiki mbili nyuma.lakini kitu ambacho kinawashangaza watu ni kwamba,hata kati ka soko gumu la siku hizi ambao mauzo ni YA ku hustle sana japo upate certified GOLD,(mauzo zaidi ya laki tano).jama ye anazidi kuchana mauzo ya platinum..kwa kumbu kumbu tuna kufahamisha ni kwamba eminem album zake zote zimegonga PLATINUM kasoro ile ya kwanza ya REAL SLIM SHADDY..
Na vile vile album yake mchiz ni kwamba inaongoza billboard top 200 albums kwa week ya pili mfululizo sasa..

KIDOGO JAYZ AMPOTEZE BEYONCE NCHINI UINGEREZA...

Habari zilizo tufikia kutoka  nchini uingereza kupitia gazette la the SUN zinasema kua mwana dada Beyonce ,alikoswa kugongwa na taxi nchini uingereza siku ya jana (juma tano)mara baada ya kufungua mlango ili aweze kutoka kwenye gari,ila kilicho msisimua ni kwamba alivyo fungua tuu , mlango alishangaa tuu mlango kuondoshwa na gari nyengine. tukio hili lilitokea wakati ndio wanataka washuke  kwenye gari aina ya mercedes benz yenye rangi ya silver ambao walikuwa wakisafiria yeye na mme we JAY-Z.
washkaji walikua wanaelekea  kufanya shopping then ndio waeleke kwenye dinner eneo liitwalo swanky London eatery, Zuma, in Knightsbridge..lakini mara baada ya tukio hili ni kwamba, Beyonce alishtuka sana na shopping haikuendelea wala nini..dah !!! mASKINI...!!! inamaana JAYZ angebaki bila bila ???  wheeeewwwwwwwww...!!! balaa..

Wednesday, July 7, 2010

GEORGE MICHAEL ALIPATA AJALI TENA SIKU YA JUMA PILI...

msani huyo mwenye umri wa miaka 47,alikamatwa majira ya kuamkia siku ya juma pili saa tisa na nusu (3:35 am) polisi wa mji wa london walipigiwa simu na watu wanao kaa eneo hilo.baada kupokea simu kwa faster polisi wali ibuka eneo hilo la ajali papo kwa hapo. japo kuwa jama alipata ajali,alishtakiwa na kwa kosa la kuendesha gari nchini  akiwa anasadikika kuwa kalewa.

msani huyo bwana GEORGE, miaka 3 ya nyuma nazungumzia mwaka wa 2007 alikatazwa kuedesha gari kwa miaka 2,mara baada ya kugonga maduka ya kusafishia picha yaliopo karibu na nyumbani kwake maeneo la leafy kaskazini mwa mji wa London.

jama katoka kwa kulipa bondi ya kiasi cha fedha ambacho hakija wekwa wazi,lakini case hiyo itaendelea mwezi wa nane mwaka huu...

Tuesday, July 6, 2010

MWANA MUZIKI DMX AMEACHIWA UHURU LEO TOKA GEREZA LA ARIZONA

X mwenye majina halisi Earl Simmons, aliwekwa ndani mwanzoni mwa mwaka huu mara baada ku vunja sharti ya probation yAKE kwa kutumia madawa ya kulevya tena. lakini asubuhi ya leo mkali huyo wa muziki wa hip hop ameachiwa uhuru toka gereza hilo.kwa kukumbusha ni kwamba ni gereza hili hilo ambao limetoa probation ya miaka 3 kwa mwana muziki mwengine nchini marekani anaetambulika kwa jina la LIL WAYNE a.k.a DWAYNE CARTER..wayne ata anza kifungo cha nje mara baada kutoka gereza la Rikers island jijini Newyork .