Thursday, July 1, 2010

BARUA YA SUGU KWA WANAINCHI



KATIKA KA BARUA YAKE SUGU Anasema HIVI.......................napenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha wananchi wenzangu wa Mbeya Mjini, wapenzi wa muziki wangu, wanachama wenzangu wa CHADEMA na watanzania kwa ujumla tarehe 28 Juni 2010 nilikamatwa na polisi kwa kile walichonieleza kuwa kuna malalamiko dhidi yangu kuwa nimemtishia kwa maneno kumuua Ruge Mutahaba kupitia wimbo uitwao “Wanna Kill” uliopo kwenye album iitwayo “Anti Virus”.

Walinikamata saa 5 asubuhi nikiwa naingia ukumbi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya kutoa Mada kuhusu “Tathmini ya Muziki wa Kizazi Kipya na Hatma yake nchini” na kunihoji kwa takrabani masaa matano mpaka saa 10 jioni.

Wameniachia kwa kile walichonieleza kuwa ‘dhamana ya kujidhamini mwenyewe’ na kunitaka niripoti kwao siku ya jumatano tarehe 30 Juni saa 5 asubuhi siku ambayo nilipanga kwenye ratiba zangu kurejea nyumbani Mbeya Mjini kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kabla ya tarehe ya mwisho ya utoaji na upokeaji fomu ndani ya CHADEMA.

Katika mahojiano nao yaliyofanyika Makao Makuu ya Upelelezi Wizara ya Mambo ya Ndani; maofisa usalama (CID) walionihoji walirejea mstari mmoja katika kiitikio cha wimbo husika wenye maneno “I Wanna Kill Right Now” na kusema kwamba mlalamikaji ameutafsiri mstari huo kuwa ni tishio la kutaka kumuua.
Napenda kuwajulisha mashabiki wangu na watanzania wenzangu kwamba nimelieza wazi jeshi la polisi kwamba hakuna wimbo wala maneno niliyowahi kutamka kwa lengo la kukusudia kumuua binadamu yoyote. Niliwaeleza jeshi la polisi kwamba sanaa ya muziki inalugha zake zake za kifasihi.

Maadhui ya wimbo mzima yamejikita katika harakati zangu za siku zote za kupambana na wanyonyaji dhidi ya maslahi ya wasanii Tanzania na wimbo huo una maudhui ya kutaka “Kuondoa ama kuiua dhamira ya mbovu na nia zao ovu”.

Ni vyema mashabaki wangu, wanachama wenzangu na watanzania kwa ujumla wakarejea katika Kamusi mbalimbali za kimataifa ambapoo neno KILL linamaana zaidi ya 10 zikibeba pia maana ya KUKOMESHA, KUONDOA nk.

Katika wimbo huo nimeghani kwa kutumia fasihi mambo ya ukweli yanayotokea katika sekta ya sanaa na wala hauna dhamira yoyote wala maudhui ya kufanya kosa lolote la jinai; hivyo kama kuna mtu ameguswa na ukweli uliomo katika wimbo huo na hakubaliani nao basi aupinge kwa hoja ama akafungue madai badala ya kukimbilia kutaka kuliingiza jeshi la polisi kwenye masuala ya sanaa.

Aidha nimeshangazwa na hatua ya jalada hilo la polisi kufunguliwa ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Wizara ya Mambo ya Ndani yaliyopo Wilaya ya Ilala wakati mimi na mlalamikaji wote ni wakazi wa Wilaya ya Kinondoni.

Baada ya maelezo niliyoyatoa ni matumaini yangu kuwa jeshi la Polisi ambalo lina kazi muhimu zaidi ya kukabiliana na ujambazi na vitendo vingine vya uhalifu ambavyo vinazidi kuongezeka katika Mkoa wa Dar es salaam ambapo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yapo litaelekeza nguvu zake katika kukabiliana na vitendo hivyo vya makosa ya Jinai badala ya kupoteza muda wake kushughulikia masuala ya kifasihi ambayo yana sura ya madai yasiyo na uzito wowote.
Lakini vile vile Kwa sasa Mheshimiwa mtarajiwa yuko Mkoani Mbeya akiwa kwenye mchakato wa kurudisha fomu baada ya kupata ridhaa ya chama chake...Sugu anaungana na wasanii wengine toka Tanzania kama Kalama Masoud AKA Kalapina anatakayegombea Udiwani jimbo la Kinondoni-DSM kupitia chama cha CUF,na Nakaaya Sumary aliyetangaza nia ya kugombea Ubunge mkoani Arusha kwa tiketi ya CHADEMA...Hatutauza kura zetu....ila Kila la Kheri waheshimiwa watarajiwa!
na hu ndio muonekana wake na wana cha wenzake akina G-solo



No comments:

Post a Comment