Tuesday, June 29, 2010

NDEGE YA JWTZ IMEANGUKA NA RUBAN KUFARIKI HAPO HAPO


Ndege hiyo ilikuwa ikitokea mkoani Tanga na inadaiwa kuwa ilibeba watu 5,Rubani ndiye alipoteza uhai,kwa mujibu wa shuhuda mwingine aliyepo eneo la tukio anasema kwa hali ya ndege ilivyo hakuna mtu aliyepona,na kwamba ndege hiyo ni ya JWTZ kituo cha Ngerengere mkoani Morogoro,mpaka sasa hali ni tete eneo la la tukio kwani hakuna gari linalokwenda wala kurudi kutokana ndege hiyo kuziba barabara.


============
Habari zilizoifikia Blog yako ya HITS FM RADIO hivi punde imehabarishwa kuwa Ndege ndogo ambayo idadi ya watu waliokuwemo bado haijajulikana, imepata ajali kwa kugongana na basi iliokuwa imebeba abiria (watalii) ambao nao idadi yao haijajulikana kwa haraharaka,maeneo ya Kabuku Mkoani Tanga.
Aidha chanzo chetu cha habari ambacho kipo kwenye eneo la tukio kimeeleza kuwa ndege hiyo iko nyang'anyang'a na haitamaniki tena, imeziba barabara na kwamba mpaka sasa ni mtu mmoja aliyebainika kupoteza maisha,aidha wananchi walioko sehemu ya tukio wanaaendelea na juhudi za kuwaokoa majeruhi ndani ya ndege hiyo halikadhalika na kwenye basi pia.


Chanzo cha habari kinazidi kusema kuwa mpaka ajali hiyo inatokea , wananchi wanajitokeza kuwasaidia majeruhi hakuna chombo chochote cha usalama kilichkuwa kimekwisha fika eneo la tukio."kwa sasa kuna msongamano mkubwa wa watu na mabasi mengi yamekwama hapa kwa saababu ndege imeziba barabara na magari hayawezi kupita"kimesema chanzo chetu cha habari.



Wanajamvini habari ndiyo hiyo lakini tutazidi kuhabarishana zaidi kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana.


No comments:

Post a Comment