Mie najiuliza kwa nini wasani wana kimbilia..nchini jirani kama kenya ,sauz,musumbiji kwenda kufanya kazi zao za kimziki wakati si wenyewe bongo kuna production houses za ukweli...msanii J1 alikaa kimya kidogo,lakini nimepata taarifa kumbe hakwepo nchini. jama alie shine sana na record yake ya kidato kimoja karudi nchini baada kwenda Nai-robbery kutengeneza ujio mpya..anadai kuwa mawe yapo tayari na tusubirie tuu kombe la dunia liishe then atugawie uonjo kutoka huko NAI..
kwa mdomo wake anasema..
"Nimerudi na nimejipanga vya kutosha na sio muda mrefu nitaanza ngoma nyingi tu nimezifanyia Kenya na nimerudi kivingine kabisa kwani hii albam yangu itakuwa imeshiba na hili zoezi la kuachia ngoma litakuwa mara tu baada ya kombe la dunia kuisha”
Katika mpango mzima wa kujipanga mtu mzima JI aliamua kujikita nchini Kenya kwa ajili ya kuwa karibu na wasanii kutoka nchini humo ambao alikuwa na mpango wa kufanya nao kolabo. “unajua ukitaka ukaribu na msanii inabidi umfute aliko ili kuepusha usumbufu wa hapa na pale”JI aliendelea kwa kusema…… “sasa hivi nakuja na albamu yangu ambayo ina jumla ya nyimbo kumi na nimebakiza kama nyimbo ne tu imalizike”
Akiongelea albamu yake ya kwanza ya kidato kimoja ambayo ameiingiza sokni hivi karibuni JI alisema “kidato kimoja ndio album yangu ya kwanza kiingiza sokoni kwa hiyo siju soko linaendaje na ukizingatia ndio kwanza ina miezi mine tu tangu niingize sokoni”
No comments:
Post a Comment