Msanii wa hip hop hapa bongo,akitokea mjini Arusha akijulikana kwa jina halisi la Jacob Makalla a.k.a JCB, hivi karibuni amekwisha ikamilisha albamu yake ijulkanayo kwa jina la Nakala za Makala yenye jumla ya nyimbo 16.
akizungumza leo mchana ndani ya kipindi cha XXL .amesema kuwa albamu hiyo iko tayari na imekwishaingia sokoni jana kwa ajili ya mauzo.
JCB amezitaja baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Movement of silence,Kijiti,Kijenge ya juu,Usinitafute,Prison break,Ninapo,arusha na nyinginezo,anasema na kuongeza kuwa albamu hiyo imerekodiwa ndani ya studio za Watengwa chini ya prodyuza David Bakari a.k.a Daz.
JCB amebainisha kuwa albamu hiyo iliyojaa kila aina ya maudhui inauzwa 10,000.
No comments:
Post a Comment