VODACOM FOUNDATION KUDHAMINI GALA NIGHT ZANZIBAR
Meneja wa Mfuko wa Vodacom fondition, Yessaya Mwakifulefule 8kushoto na mbunifu wa mavazi Mstapha Hassanali wakizungumza na waandishi wa habari
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na mbunifu wa mavazi Mstapha Hassanali imejitokeza kudhamini maonesho ya mavazi ya hisani yanayolenga kuboresha hali ya mazingira ya Hospital ya wenye matatizo ya akili ZANZIBAR.
Maonesho hayo yanayofahamika kama 'Fashion 4 Health Black and Gold Gala' yanafanyika mara ya tatu mfururizo yanaandaliwa na Exprlore ZANZIBAR yatafanyika tarehe 30 Julai mwaka huu katika Hotel ya Serena Inn Mjini humo.
"Kwa kuthamini umhimu wa jamii ambayo tunafanya nayo kazi na kwa Heshma ya Maryam Olsen wa Explore Zanzibar tumeshawishika kudhamini onesho hili kuchangia majengo ya Hospitali hiyo," alisema Mwakifulefule.
Naye mbunifu maarufu wa mavazi nchini Mstafa Hassanali alisema katika maonesho hayo atazindua mtindo wake mpya wa mavazi unaofahamika kama 'KARAFUU Collections', akiambatana na wanamitindo wengine 10 kutoka Tanzania bara wakisindikizwa na burudani kutoka katika bendi ya Tanzanite.
Alisema mbunifu mwingine wa Mavazi Farouque Abdella wa zanzibar atafungua pazia la maonesho hayo akifuatiwa na mbunifu Mago ambapo wadhamini mbalimbali wakiwemo PSI Tanzania, 361 degree Events na Mstapha Hassanali Couture wamejitokeza kudhamini maonesho hayo.
"Wagonjwa wana kila sababu ya kujifunza na kuishi katika mazingira ya kupendeza lakini tunahitaji msaada na mimi kwa kushirikiana na wenzangu tutashiriki kikamilifu katika onesho hilo kuchangisha fedha," alisema hassanali.
No comments:
Post a Comment