Friday, February 25, 2011

PREZZO AISHIWA....!!!!!


Hip-Hop artist toka Kenya,Jackson Makini Ngechu aka Cash Money Brothers aka CMB Prezzo kwa sasa inasemekana amechoka kiuchumi.
Kwa sasa CMB Prezzo,mzee wa swagga mambo yake sio safi na inasemekana kuwa hana hata sehemu ya kulala coz amehamia kwa mshikaji wake pande za Hurlingham kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kukorofishana na mjomba wake ambaye ndio alimpatia nyumba ya kuishi na hana sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kurudi nyumbani kwa mother wake.
Prezzo na familia yake waliachiwa urithi toka kwa baba yao na inadaiwa kuwa Prezzo amezitumia vibaya mali zilizoachwa na baba yake Marehemu Mzee Makini Ngechu.

No comments:

Post a Comment