Friday, February 25, 2011

KIBA ALALAMA KUITWA MBANA PUA KWA WALE WOTE WANAO IMBA STYLE KAMA YAKE

KIBA ANASEMA KUA .JAMII INATAKIWA ITAMBUE MCHANGO WAO KWA JAMII ..NA ANAOMBA WATU WASTISHE MARA MOJA KUWAITA WABANA PUA KWA KILE ALICHO DAI KUA NI KUWA KUWAZALILISHA NA KUWAPUNGUZIA HESHIMA..

USHAURI TOKA KWA WANENE WA BURUDANI NDANI YA DASLAM


1_Fa
Mwana Fa, yeye alishauri kuwepo na asilimia kubwa ya ya watu wanaoujua muziki (Academy) kuchagua mtu analiyefanya vizuri katika kazi nzima, ili kila mmoja apate haki yake kutokana nakazi yake, kwani anaamini upigaji wa kura watu wengi huchakachua katika kupiga kura, kwa kutumia tovuti simu na magazeti, hivyo zipewe kiasi kidogo cha asilimia.

100_1957
Man Water naye hakuwa na imani juu ya upigani kura, kwani aliamini uchakachuaji utakuwa mkubwa, na ili kuondoa huo uchakachuani, alikuwa na maoni kwamba watanzania wakapige kura kama vile wanavyochagua raisi.
isha
Isha Ramadhani,  yeye alikuwa na maoni kwamba wasanii wakongwe kama wakina Hadija Kopa, kutowachanya na wasanii wachanga (Wabongo Fleva), kwakuwa hao wameanza kuimba hata kabla ya wao hawajazaliwa. sasa wanapomshindanisha na msanii mchanga na anaposhindwa ni sawa na kumdhalilisha, anaomba washindanishwe na 'Manguli' wenzake ambao wapo kwenye' Gemu' muda mrefu.
Mpoto
Mrisho Mpoto, yeye alikuwa anamaoni kwamba, watu wachache wanaoujua muziki (Wadau) wakiwa pamoja ilikufanya kazi hiyo, basi uchakachuaji ndiyo utakuwa mkubwa zaidi. anaamini kwamba mtu akiwa na wadau wake kadhaa, anaowamiliki na kuongea nao ni rahisi kupitishwa kuwa mshindi bila ya hata vigezo stahiki.
Fid
Ngosha the King Dom, ama Fid Q mtoto wa Kubanda naye alisema kwamba hata New York Marekani watu wanachakachua kutokana na wingi wa laini za Simu, kwa hiyo bado alimuunga mkono Mwana Fa kwamba lazima wadau wanaoujua mziki, waweze kuwa makini kuangalia kazi ya mtu na kutenda ile haki na mtu kupata anachostaili kutokana na kazi yake.
100_1999
Kwa upande wa Ali Kiba 4 realy yeye alikuwa na maoni kwamba, hii tabia ya kuitana wabana pua, sasa anaombwa kuonyesha wabaniwa pua ni akina nai?. anasema tabia hii imekuwa inamkera sana, kwani anahisi huku sio kusaidia muziki ila ni kutengeneza mitafakano baina ya wasanii na kugawa makundi ya watu na wasanii katika uimbaji  100_2022
Kwa upande wa Mpoki aka yake ikiwa kwenye shati lake yeye alikuwa akiuliza juu ya kuwepo kufuta jasho kwa wale ambao watakosa tuzo yoyote, kwani watahitaji kupata chochote kutokana na vile vijisenti walivyotuma kwenye Sms zao.

MDADA ''SHAA'' ALIE TUPIA SHOGA..KUIBUKA NA KIDEO KIINGINE...

Msanii anayetikisa kunako Bongo Flava Sarah Kaisi anyejulikana kwa jina la kisanii kama Shaa, Amemaliza kufanya video yake mpya ambayo hakutaja inakwenda kwa jina gani lakini alisema kwamba imefanywa na kusimamiwa na Adam wa Visual LAB. Shaa ameongeza kwamba video itakua hewani baada ya wiki chache na amewataka mashabiki wake kukaa tayari kwa video yake hiyo

CONCERT LA ALBINO FLANI NDANI YA MAREKANI

PREZZO AISHIWA....!!!!!


Hip-Hop artist toka Kenya,Jackson Makini Ngechu aka Cash Money Brothers aka CMB Prezzo kwa sasa inasemekana amechoka kiuchumi.
Kwa sasa CMB Prezzo,mzee wa swagga mambo yake sio safi na inasemekana kuwa hana hata sehemu ya kulala coz amehamia kwa mshikaji wake pande za Hurlingham kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kukorofishana na mjomba wake ambaye ndio alimpatia nyumba ya kuishi na hana sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kurudi nyumbani kwa mother wake.
Prezzo na familia yake waliachiwa urithi toka kwa baba yao na inadaiwa kuwa Prezzo amezitumia vibaya mali zilizoachwa na baba yake Marehemu Mzee Makini Ngechu.